Menejimenti ya VETA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore, leo, tarehe 7 Machi 2025 imetembelea kiwanda cha Emirate Alluminium Profile kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu kuhusu namna ufundi wa Aluminiamu unavyofundishwa sehemu ya kazi.

Ziara ililenga pia kuona namna ya kuanzisha ushirikiano kati ya VETA na Emirate Alluminium Profile ili kuwezesha wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya VETA kupata ujuzi zaidi kuhusiana na ufundi wa Aluminiamu kupitia mafunzo ya mahala pa kazi.

Account details will be confirmed via email.